West Brom yavurumishiwa 3-1 na Newcastle

Newcastle ikionesha kandanda safi ilifanikiwa kuilaza West Brom na kufikisha pointi sawa 50 na wanaoshikilia nafasi ya tano Chelsea.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Papiss Demba Cisse aibuka shujaa wa Newcastle

Mkwaju wa pembeni wa Hatem Ben Arfa kwa Papiss Cisse ulikuwa ni bao la kwanza kwa Newcastle ambapo alifunga bao kwa urahisi huku wachezaji wa West Brom wakidhani ameotea.

Baadae alikuwa Ben Arfa aliyeipangua ngome ya West Brom na kuandika bao la pili kabla hajamlisha pande zuri Cisse na kuandika bao la tatu ambapo mlinda mlango wa West Brom Ben Foster aliachwa akigaagaa.

Kipindi cha pili kujichanganya kwa safu ya ulinzi ya Newcastle kulimpatia nafasi Shane Long kufunga bao pekee la kufutia machozi kwa West Brom, lakini Newcastle ilifanikiwa kulinda mabao yake na kujizolea pointi tatu na kujiweka katika mazingira mazuri ya kucheza ligi ya Ulaya msimu ujao.