Kalou hana uhakika wa kuwa na Chelsea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Solomon Kalou akiwa na Drogba

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na Chelsea Salomon Kalou hakutoa tamko la wazi alipoulizwa kama angependa kandarasi yake iongezwe baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Aliifungia Chelsea goli la pekee dhidi ya Benfica siku ya Jumanne katika robo fainali ya kwanza katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.

"Kwangu jambo muhimu kwa sasa siyo kutafuta kandarasi mpya, ni kuwa na burudani kwa sasa na kucheza kadiri ya uwezo wangu pamoja na kusaidia timu kushinda mechi zilizobakia," alisema.

"Nikifanya hivyo, nitafurahi sana."

Mchezaji huyo amekua na timu ya Chelsea tangu kutoka klabu ya Feyenoord mwaka 2006, lakini huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu wakati kandarasi yake itakapomalizika.

Mwaka uliopita Kalou alisema alitaka kupata hakikisho la kucheza mechi nyingi akiwa na Chelsea kabla kutia saini kandarasi mpya.