Comolli aondoka Liverpool

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Damien Comolli aondoka Liverpool kwa sababu za kifamilia

Mkurugenzi wa kandanda wa Liverpool Damien Comolli ameondoka katika klabu hiyo,timu ya Liverpool imetangaza.

Comolli alichaguliwa kwenye nafasi hiyo na baadhi ya wamiliki wa klabu John W. Henry na Tom Werner kufuatia wao kuchukua timu Septemba mwaka 2010.

Katika wakati wake waliweza kumnunua mchezaji Andy Carroll kwa pauni za Uingereza milioni £35 na Luis Suarez kwa pauni za Uingereza milioni £22.7.

Comolli alisema: "Nimefurahi kuondoka kwenye klabu hii na kurudi nyumbani Ufaransa kwa sababu za kifamilia."

Aliongeza: " Nimefurahi kupewa fursa ya kufanya kazi Liverpool. Naitakia timu hii kila la heri."

Tangazo hilo limetolewa wakati Liverpool ikijiandaa kwa mechi yake ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Everton siku ya Jumamosi katika uwanja wa Wembley.

Comolli, mwenye umri wa miaka 39, alichaguliwa kujiunga na Liverpool Novemba mwaka 2010 kushirikiana na Meneja wa zamani wa timu hiyo Roy Hodgson.

Wakati huo Comolli alisema kuwa Hodgson, mtangulizi wa Kenny Dalglish, ndiye aliyekuwa na uamuzi wa mwisho juu ya kuhama kwa wachezaji.

Alisema jukumu lake ilikuwa ni kutambua wachezaji na hii ni kumaanisha kuwa alikuwa na jukumu la kuangalia matumizi ya pauni za Uingereza milioni £112.8m mwaka uliopita.