Arsenal yanyolewa nyumbani

Image caption Arsenal washangilia bao lao

Wigan ilithibitisha kuwa walipoifunga Manchester United haikuwa ajali.

Jumatatu usiku Arsenal ilipigwa nyumbani 2-1 na Wigan ambayo inapigania kubakia ligi kuu ya Premier.

Kwa ushindi huo sasa Wigana inashikilia nafasi ya 16 katika jedwali la ligi ya Uingereza.

Arsenal ilikuwa inatafuta ushindi utakayoihakikishia kuwa wako alama nane mbele ya Spurs.

Licha ya kufungwa huko Arsenal bado wako katika nafasi ya tatu , nyuma ya Manchester United na Manchester City.

Bao la kwanza la Wigan lilifungwa na Franco di Santo katika dakika ya saba na dakika moja baadaye Jordi Gomez akaongeza la pili

Thomas Vermaelen aliipatia timu ya nyumbani, Arsenal bao lao moja.