Kombe la Olimpiki lauzwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kombe la fedha la Olimpiki

Kombe la fedha ambalo lilitunikiwa mshindi wa kwanza wa mbio za Olimpiki katika marathon limeuzwa katika mnada kwa takriban dolla laki tisa za Kimarekani ikiwa ni bei ya juu zaidi kwa kifaa chochote cha Olympiki.

Mbio hizo zilibuniwa hasa kwa michezo ya kwanza ya Olympiki mjini Athens mnamo mwaka 1896,zikihamasishwa na ngano za Wayunani wa kale.

Kombe hilo liliuzwa na mjukuu wa aliyetunukiwa kombe hilo ,Spyros Louis kutoka Ugiriki. Mnada huo ulifanyika mjini London siku mia moja kamili kabla ya jiji hilo kua mwenyeji wa michezo ya Olympiki mnamo mwezi wa Julai.