Real Madrid yafungwa

Bao lililofungwa katika dakika za mwisho na Mario Gomez iliiweka Bayern Munich kifua mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mario Gomez akiipatia Bayern Munich bao la pili

Ushindi huo ni katika duru ya kwanza ya mechi ya nusu fainali ya kombe la mabingwa bara ulaya.

Mshambulizi Franck Ribery alikuwa wa kwanza kuona lango la Real Madrid pale alipofumua mkwaju mkali na kumuacha kipa Iker Casillas akiwa hoi.

Lakini dakika sabu tu baada ya kipindi cha pili kuanza Mesut Ozil akiwa hauta chache toka langoni aliipatia bao lake.

Wengi walifikiri mechi hiyo huenda ikaishia kwa sare ya 1-1 kabla ya Gomez kuchafua mambo dakika za mwisho.

Kabla ya kufunga bao hilo Gomez alipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Hata hivyo mwamba wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hakua na siku njema kwani hakuna kubwa alilofanya akiwa uwanjani.