Kenya yatangaza kikosi cha Marathon

Imebadilishwa: 25 Aprili, 2012 - Saa 14:10 GMT

Chama cha michezo ya riadha nchini Kenya kimetangaza orodha ya wanariadha watakaowakilisha Kenya katika michezo ya Olimpiki ya mjini London baadaye mwaka huu.

Wilson Kipsang

Wilson Kipsang mjini London

Miongoni mwa waliotajwa ni Wilson Kiplagat ambaye alishinda mbio za Marathon ya mji wa London siku ya Jumapili iliyopita na mshindi wa mara mbili wa mashindano ya dunia Abel Kirui pamoja na Moses Mosop aliyemaliza wa tatu kwenye mbio za Rotterdam mwezi huu.

Hata hivyo Patrick Makau anayeshikilia rekodi ya dunia ametupwa nje baada ya kushindwa kumaliza mbio za London Marathon siku ya Jumapili.

Washindi watatu kushiriki

Washindi wa London kushiriki London 2012

Kwa upande wa wanawake, washindi waliochukua nafasi tatu za mwanzo katika mbio za London Marathon Mary Keitany, mshindi wa dunia Edna Kiplagat na Priscah Jeptoo wamechaguliwa kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki ya London mwaka 2012.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.