Mfumo mpya kugundua dawa

Mbinu kabambe
Image caption Mpango wa pasipoti

Mwanariadha wa mbio za masafa marefu kutoka Ureno amekua mimbiaji wa kwanza kusimamishwa kwa kosa la kutumia dawa ya kuongeza nguvu mwilini kupitia mpango uliopewa jina pasipoti bayolojia.

Shirika linaloongoza michezo ya riadha duniani, IAAF limesema kua Helder Ornelas mwenye umri wa miaka 38 amepigwa marufuku ya kutoshiriki mbio na Chama cha Ureno kwa kipindi cha miaka minne.

Ornelas ambaye ameshiriki mashindano ya Olimpiki mara mbili, alikumbwa na kikwazo kufuatia mfululizo wa majaribio ya damu iliyokusanywa na IAAF kati ya mwezi disemba mwaka 2008 na Novemba 2010.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha asimamishwe kwa kutegemea ushahidi huu wa kupitia tabia na nyenzo za mkimbiaji kupitia kipindi fulani katika kukabiliana na tabia ya matumizi ya dawa za kuongezea nguvu mwilini.

Image caption Juhudi kupambana na dawa

Mpango wa pasipoti huchunguza damu ya mwanariadha kwa kipindi fulani kuchunguza ushahidi wa aina yoyote wa kama alitumia dawa hio.

Mpango huu ulianzishwa na chama cha waendesha baiskeli,USI, pamoja na shirika linalopambana na matumizi ya dawa za kuongezea nguvu mwilini kimataifa mnamo mwaka 2008. Chama cha kuogelea ni miongoni mwa mengine yanayotumia mfumo huu pia.

FIFA pia inajaribu mpango huu katika soka.