Di Mateo ahakikishiwa kujadili Chelsea

Di Matteo Haki miliki ya picha AP
Image caption Roberto Di Matteo

Kocha msaidizi wa Chelsea Roberto Di Matteo amehakikishiwa leo kua uwamuzi juu ya nafasi yake katika klabu huio utafanywa baada ya fainali ya Klabu bingwa.

Kuna tetesi kua Mkufunzi huyo wa mda amekua na unyonge wa kiasi akihisi kua Klabu hio ina mipango ya kumpokonya wadhifa wa kua Meneja wake na badala yake wamtafute mtu niwngine, hata ikiwa matokeo ya mechi dhidi ya Bayern Munich yatakua mazuri.

Lakini akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa ushirika wa klabu hio na timu ya magari ya mbio za Langalanga ya Sauber, Mkurugenzi mtendaji Ron Gourlay ameliambia shirika la habari Press Association kua, Klabu hio ina imani kubwa na Kocha huyo tangu ajiunge nao kama meneja wa mda na kwamba watafanya tathmini yao mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo, Gourlay alishindwa kujibu kama Di Matteo amefanya kazi ya kutosha kuwekwa kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya Meneja wa klabu.

Hata kabla ya kufuzu kushiriki fainali ya Ligi ya mabingwa, mashabiki wengi walimuunga mkono Di Mateo achaguliwe kumrithi Andre Villas Boas.

Licha ya imani zote hizo, endapo Di Mateo atashindwa kuwika mjini Muinich,basi Abramovich ataitumia kama sababu ya kumuondoa Di Mateo ambaye atakua ameshindwa kuipandisha Chelsea kutoka nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Premiership na hivyo kukosa michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya mwakani.