Yaya Toure ataka City iwe bora duniani

Yaya Toure Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yaya Toure

Yaya Toure ameiambia BBC michezo kua anataka kuisadia klabu yake ya Manchester City iwe klabu bora duniani.

Mcheza kiungo huyo amekua kiini cha klabu hio msimu huu, klabu ambayo wikendi hii inadhamiria kushinda kombe la Ligi ya Premier ya England.

Yaya amesema kua, sababu iliyonileta hapa ni kuisadia timu.......kusaidia katika kuiendesha mbele na kuifanya iwe kubwa kuliko zote duniani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yaya Toure

City inaipokea QPR siku ya Jumapili na ikishinda mechi hiyo wakati Manchester United ikishindwa kushinda Sunderland kwa angalau mabao kumi basi City itatawazwa bingwa wa msimu wa mwaka 2011/2012.

Alipoulizwa kama ameanza kuhisi shinikizo za pambano hilo la mwisho, Toure aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 24, alijibu hapana, kwa sababu nina uzowefu. Nimeisha shiriki michuano kama hii na kushinda vikombe kadhaa.

Toure, alikua na klabu ya Barcelona iliyoshinda vikombe sita vya nchini na nje ya nchi mwaka 2009 na amekua kishawishi kikubwa msimu huu kwa Manchester city.