Miujiza inawezekana asema Evra

Patrice Evra
Image caption Patrice Evra-ana imani

Beki na nahodha wa klabu ya Manchester United Patrice Evra bado ana imani klabu yake inaweza kuondoka na ushindi wa Ligi kuu.

United, ikiwa katika nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli tu, inahitaji kuiona City ikijikwaa dhidi ya QPR au uwezekano wa kuimiminia Sunderland mabao yasiyopungua tisa ili kuiondoa City kileleni kwa hio tofauti ya magoli manane.

Evra anasema, huenda watu watadhani nimechanganyikiwa, lakini ni imani niliyo nayo.

"naelewa kua hatma ya matokeo haimo mikononi mwetu. Lakini ikiwa tunataka kubaki na imani ya miujiza lazima tuishinde Sunderland."