Hamilton kuongoza mbio za Uhispania

Alonzo Hamilton na Maldonaldo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alonzo Hamilton na Maldonaldo

Dereva wa timu ya magari ya McLaren katika mbio za Langalanga, Lewis Hamilton ameshinda nafasi ya kuanza mbio za jumapili za nchini Uhispania mbele ya Madereva ambao hawakutarajiwa kua katika nafasi za juu Pastor Maldonado na Fernando Alonso.

Hamilton aliweka mda bora wa tafauti ya sekunde 0.578 kati yake na dereva wa timu ya Williams ya Maldonado, huku Alonso akizidisha mda wake kwa kasi zaidi akijiweka mstari wa mbele.

Bingwa mtetezi wa mashindano haya Sebastian Vettel amemaliza katika nafasi ya nane baada ya kushindwa kuweka mda mzuri katika mbio za mwisho za kuchuja.

Dereva wa pili wa timu ya McLaren Jenson Button pamoja na wa timu ya Red Bull Mark Webber walimaliza katika nafasi ya 11 na 12th.

Hivyo madereva hao wakakosa kutokana na sababu tofauti - Button alihangaishwa na usukani wa gari lake na Webber alishindwa kwa sababu mafundi walidhani mda wake katika mbio za awali ulitosha kumsogeza mbele katika mbio za mwisho.

Lakini hilo halikutokea na badala yake Madereva wengine walijiwekea mda mzuri na bora kuliko uliowekwa katika mbio za mapema. Hali hio ikamuondoa Webber katika 10 bora.