Mancini asema ana imani na vijana

Meneja wa klabu ya Manchester city Roberto Mancini anasema ana imani na wachezaji wake kutimiza jukumu lao na kuvishwa kilemba cha Mabingwa wa msimu huu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Roberto Mancini

Hata ikiwa watashindwa,Mancini amesisitiza kua vijana wake wamecheza soka safi msimu huu wa Ligi kuu.

Roberto Mancini amesema: Nawaamini kwa asili mia 100. Wanafahamu vyema kua ushindi wa Ligi na kuin'goa United kutoka kilele cha soka ilichoshikilia kwa mda mrefu ni jukumu lao.

Aliongezea kusema kua' wamejitahidi na kupambana kila wanapoingia uwanjani katika Ligi ambayo ni mojapo ya Ligi kali duniani.

Mancini amemalizia kwa kusema ninavyohisi ni kwamba mwishoni ni mshindi ni yule anayestahili ushindi''

Klabu ya City iliongoza ligi kwa pointi 8 na kujikuta nyuma ya mahasimu wao Manchester united kwa pointi 8 baada ya kufungwa kwenye uwanja wa Arsenal tareh 8 mwezi Aprili.

Manchester City inapambana na QPR kwenye uwanja wa Etihad huku United ikielekea uwanja wa Brittania kuchuana na Sunderland.

Mancini anasema kua "nadhani kwa wakati huu ilikua bora kwentu kupoteza mechi dhidi ya Arsenal, kwa sababu hilo lilitupunguzia shinikizo''

Daima tumeamini, na kuendelea kucheza soka safi licha ya kua na matatizo kipindi cha mwezi mmoja tu.

Image caption Adel Tarabti

"tulipocheza dhidi ya Manchester United na Newcastle tulicheza vizuri sana, dhidi ya Timu ambazo ni kubwa na zinazocheza mchezo wa kiwango cha juu, nadhani hali itakua hio hio dhidi ya QPR.

Ferguson na Meneja wa QPR Mark Hughes wamezielezea mbinu za Mancini kama za kuzuia, ambapo Ferguson anadai kua walipocheza dhidi ya City ilitumia wacheza kiungo watano.