Serena amshinda Azarenka

Serena Williams Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serena Williams

Serena Williams amemshinda mchezaji anayeshikilia namba ya kwanza kama mchezaji bora duniani Victoria Azarenka 6-1 6-3 kushinda mashindano ya Madrid Open kwa mara ya kwanza.

Hii ni mara ya kwanza kwa Serena Williams kushiriki mashindano barani Ulaya msimu huu na mchezaji huyo ambaye ameshuka hadhi hadi namba sita alimiliki mchezo msima kwa seti zote mbili.

Mchuano uliendelea kwa zaidi ya saa moja ambapo Mmarekani aliibuka mshindi na kuthibitisha kiwango chake cha uchezaji kua bora akitazamia kushiriki mashindano ya Ufaransa, French Open yanayoanza Mei 27.

Image caption Victoria Azarenka

Ushindi pekee wa Azarenka mbele ya Williams ulitokea mwaka 2009 kwenye fainali ya mashindano ya Miami, lakini hiyo ni historia ambayo Mmarekani hakutaka kukumbushwa.

Mashindano haya ya Madrid Open ni ya pili mfululizo ya vumbi kwenye ratiba ya WTA kwa Williams kushinda, siku chache baada ya kushinda ya huko Charleston