Maldonado ashinda mbio za Uhispania

Pastor Maldonado
Image caption Pastor Maldonado

Pastor Maldonado, akiwa ni raia kutoka Venezuela na dereva wa timu magari ya Williams, ameshinda mashindano ya magari ya langalanga kwa mara ya kwanza kabisa akimpiku dereva wa timu ya magari ya Ferrari Fernando Alonso.

Maldonado, akishiriki msimu wake wa pili, ameshinda mashindano ya Uhispania kwa kutumia ujanja wa kusimama kituoni mara chache na kutumia muda mfupi kuliko Ferrari.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Pastor Maldonado na Williams

Mwishoni Alonso aliponea chupuchupu kupitwa na gari la timu ya Lotus, Kimi Raikkonen, aliyemaliza wa tatu.

Dereva wa timu ya magari ya McLaren, Lewis Hamilton, alishinda mbio za mchujo lakini akaadhibiwa kwa kuegesha gari lake kando mwa njia ya magari kwa sababu hakuwa na mafuta ya kutosha alipambana kiume kutoka nafasi ya 24 akimaliza wa 8, huku dereva mwenzake Jenson Button akimaliza nyuma yake katika nafasi ya 9.

Alonso aliyemaliza wa pili amejiweka katika nafasi ya kwanza kwa kuwa na pointi sawa na dereva anayeongoza kwa pointi nyingi Sebastian Vettel, aliyemaliza wa sita.