Mchezaji Patrick Mafisango afariki

Haki miliki ya picha video
Image caption Wachezaji soka wa Rwanda mazoezini

Mashabiki wa soka nchini Rwanda wanaomboleza kifo mchezaji soka wa kimataifa kutoka nchini humo Patrick Mafisango, mwenye umri wa miaka 32.

Mafisango, alikuwa amechaguliwa kuchezea kikosi cha kitakachowania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Algeria.

Alifariki katika ajali ya barabarani asubhi ya kuamkia leo mjini Dar es Salaam Tanzania.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati, anayechezea kilabu ya Simba nchini Tanzania, ndio alikuwa amerejea tu kutoka Sudan ambako timu yake ilishindwa katika michuano ya kuwania kombe la Confederation mwsihoni mwa wiki.

Kocha wa kilabu hiyo ameelezea kuhuzunishwa sana na tukio hilo.

Mafisango alifariki katika ajali iliyohusisha pikipiki na gari wakati gari alipokuwa anaenesha lilipoteza mwelekeo na kuanguka kwenye mtaro.

Alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi msimu huu wa mechi za ligi ya Tanzania kwa kuingiza magoli, 12 na aliitwa na kocha Sredrojevic kushiriki mechi ya kufuzu kwa michauano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi ujao.