Arjen Robben ajuta kukosa mkwaju

Arjen Robben Haki miliki ya picha 1
Image caption Arjen Robben

Mchezaji wa Bayern Munich ambaye zamani aliichezea Chelsea, Arjen Robben amekiri kua kukosa ule mkwaju wa penati lilikua ''balaa".

Mchezaji huyo kutoka Uholanzi alisema, sikupiga vizuri peneti ile. Nilitaka niupige mpira na nguvu nikilenga upae kidogo lakini haukuweza kupaa nilivyokusudia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bayern

"siwezi kusimulia ninivyojihisi kwa maneno lakini ni wakati mgumu kweli."

Fursa ya Robben kupiga mkwaju huo ilitokea baada ya Drogba kumkwatua Frank Ribery ndani ya eneo la hatari, lakini Petr Cech akaokoa mpira ule.

Robben alitulizwa kiwewe cha kukosa na kubembelezwa na Drogba pamoja na Michel Platini baada ya mikwaju iliyomalizika kwa ushindi wa Chelsea wa 4-3.

Robben alisema baadaye kwamba"Ukweli ni kwamba licha ya Drogba na Platini kunipa maneno mazuri, nashukuru, lakini muhimu nilitaka ushindi na kombe hilo.

Meneja wa Bayern Jupp Heynckes alimuunga mkono Robben alipokataa kushiriki mikwaju ya mwisho.