Luis Moreno agombea nafasi FIFA

Luis Moreno Ocampo
Image caption Luis Moreno Ocampo

Mwanasheria mkuu wa Mahakama ya Kimataifa inayosikiliza kesi za makosa ya jinai, Luis Moreno Ocampo ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Mkuu wa kundi la upelelezi kwenye makao makuu ya FIFA.

Msemaji wa mwenyekiti wa Kamati ya utawala huru ya FIFA, Mark Pieth, amethibitisha habari kua raia huyo wa Argentina ni miongoni mwa wagombea wa nafasi hio, ikiwa ni sehemu ya wimbi la mageuzi yenye lengo la kukabiliana na rushwa pamoja na ufisadi.

Pieth, ambaye ana sifa ya kua mtaalamu wa masuala ya utawala, ndiye anayewajibika na kuwazsilisha orodha ya wagombea wanaostahili kwa kamati kuu ya FIFA.

Wanachama wa Shirikisho walikubaliana kwa kura mjini Budapest wiki iliyopita kuunda tume ya nidhamu, pamoja na uchunguzi wa kina na pia afisi ya maamuzi.

Watakashinda nafasi hizo watatangazwa tarehe 29 Juni.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption FIFA

Mageuzi haya yalipendekezwa baada ya madai upendeleo na rushwa kutumika katika kupanga mashindano ya Kombe la dunia la mwaka 2022 katika Taifa la Ghuba la Qatar.