Liverpool yapata Meneja mpya

Brendan Rodgers Haki miliki ya picha Getty
Image caption Dalglish na Brendan Rodgers

Brendan Rodgers aliwahi kujielezea binafsi kama ''mvinyo tofauti'' na Mameneja wengine wa Uingereza.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 39 alishindwa kuongezea tu kua ni mtu maalum, kama mtu anayemuenzi Jose Mourinho alivyofanya mwaka 2004, lakini meneja huyu shupavu asiyekua na maneno mengi ameonyesha dalili za kutofautiana na wenzake Uingereza.

Rodgers alitazamiwa kutangazwa rasmi kama Meneja wa nne wa Liverpool katika kipindi cha miaka miwili akitia sahihi mkataba wa miaka mitatu.

Hii ni ishara ya hatua muhimu kwa upande wake kiongozi huyu wa michezo mzaliwa wa Ireland ya kaskazini ambaye hatazamiwi kuiona hatua hii kama itakayomsumbua.

Kwa kipindi cha misimu miwili ya mashindano ya soka Rodgers alikua na afisi ndogo katika uwanja wa mpira wa Liberty. Afisi hiyo finyu ilikua katikati ya ukumbi wenye mitambo ya kamari, kompyuta, meza na kabati.

Ingawa aliongoza kutoka afisi ndogo, hivi sasa makubwa yanayomsubiri ni makubwa kama sifa ya uwanja wa Anfield ilivyo, mashabiki wake na mahitaji yao.

Kibarua kinachomsubiri ni kikubwa. Lakini Rodgers anajiamini na amekua hivyo hata wakati akicheza soka na kustaafu akiwa mdogo m,wenye umri wa miaka 20.

Wakati akikua huko Ireland ya kaskazini, Rodgers alipenda jinsi timu za Brazil na Uholanzi za miaka ya 70 zilivyocheza na kupendwa na Babake Malachy.

Tangu hapo akageuka kua beki wa kuaminika. Majaribio aliyoyafanya katika kutaka kujiunga na Manchester United miaka ya kati ya 80 yalifanyika na kupita.

Lakini akiwa na umri wa miaka 16 Rodgers alijiunga na klabu ya Reading.

Ni wakati huu ambapo alianza kuelewa kua hakua na kipaji cha kucheza kandanda kwa kiwango cha juu ingawa safari yake ya uchezaji ilikatizwa na majeruhi bila kushiriki mechio yoyote na klabu ya Reading.

Haki miliki ya picha huw evans agency
Image caption Swansea v Tottenham

Wakati huo alikua na umri wa miaka 20, ana mke anayetarajia mtoto, lakini hakua na sababu ya kubabaika.

Moja kwa moja alianza kuwania leseni ya kufundisha soka na alipofuzu akiwa mwenye umri wa miaka 22, alikabidhiwa wadhifa wa mkufunzi wa akademia ya vijana katika klabu ya Reading.

Magharibi alifundisha katika shule za huko Reading, huku akitumia kila fursa ya kupeleleza soka ya Uhispania kujinoa zaidi.

Huko Uhiospania alitumia mda mrefu na klabu ya Barcelona,Seville,Valencia pamoja na huko Uholanzi akijitahidi kunoa mbinu zake za kuunda na kupanga timu.

Miongoni mwa wengi waliokua kivutio chake ni aliyekua kocha wa Barcelona hivi karibuni, Pep Guardiola na ni mbinu zake alizotumia katika kupanga klabu yake.

Punde si punde kipaji chake kikatambuliwa na Steve Clarke, aliyekua miongoni mwa wahudumu wa klabu ya Chelsea. Clarke alimpendekeza kwa Mourinho, ambapo Rodgers alialikwa kuunda mpango wa vijana.

Kutoka hapa, alipanda na kua kocha wa timu ya wachezaji wa akiba. Mourinho kwake Rodgers akawa kishawishi kikubwa kama alivyoelezea mwenyewe Rodgers akizungumza kuhusu wakati wake akiwa Chelsea.