Chris Hughton meneja mpya Norwich City

Klabu ya Norwich City imemteua meneja wa Birmingham City, Chris Hughton kuwa meneja wake mpya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chris Hughton meneja mpaywa Norwich City

Hughton, mwenye umri wa miaka 53, aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Newcastle, alikuwa meneja wa Birmingham tangu mwezi wa Juni mwaka 2011na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Paul Lambert.

Hughton ambaye enzi zake za kusakata kandanda aliwahi kuichezea klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland akicheza nafasi ya ulinzi, alifanikiwa kuifikisha Birmingham katika hatua ya kucheza mechi za mwisho kuwania kupanda ngazi ya Ligi Kuu ya England msimu uliopita ambapo walitolewa na Blackpool.

Norwich hawakuwa na meneja tangu Lambert alipoondika katika klabu hiyo na alitangazwa kushika hatamu za kuinoa Aston Villa tarehe 2 mwezi huu wa Juni.

Kupitia mtandao wa kijamii wa tweeter klabu ya Birmingham iliandika: "Klabu ingependa kumshukuru Chris Hughton na kikosi chake kwa jitahada walizoonesha kwa muda wa miezi 12. Kazi ya kumsaka meneja mpya imeanza."