Wachezaji wa Afrika Euro 2012

Viwanja vya mashindano
Image caption Viwanja vya mashindano

Mashindano ya kombe la Mataifa ya Ulaya, yajulikanayo kama Euro 2012 yameanza nchini Poland na Ukraine. Mashindano haya ni kivutio kwa wachezaji nyota wanaoshiriki Ligi bora za soka Duniani. Jambo la kushngaza ni kwamba kuna baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika wanaoziwakilisha nchi walizoamua kua nchi zao.

Mamilioni ya mashabiki kutoka kote barani Afrika kuanzia jana walitazamiwa kuganda kwenye viti macho kwenye runinga na masikio kwenye Rediyo kufuatilia jazba la Euro 2012.

Ingawa mashindano haya ni ya Mataifa ya Ulaya, wanashiriki wachezaji wa Afrika pia. Inakuaje Wachezaji wa Kiafrika kushiriki Kombe la Mataifa ya Ulaya?

Sababu ni kwamba baadhi ya wachezaji walizaliwa barani Afrika lakini wameamua kuyachezea Mataifa ya Ulaya ambako wanaishi na kuyageuza kua nyumbani au wazazi walizaliwa Afrika na kuhamia Ulaya lakini wakaamua kuyacfhezea Mataifa waliochagua kua nyumbani kwao.

Wachezaji hawa wangeweza kuzichezea nchi walikotoka lau kama wangependa.

Image caption Ufaransa ina kikosi cha Waafrika wengi

Ufaransa ndio nchi yenye wachezaji wengi wenye asili ya Kiafrika kwenye mashindano haya ya Euro ikiwa na jumla ya wachezaji tisa.

Miongoni mwao ni kipa Steve Mandanda ambaye asili yake ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Beki wa Manchester, Patrice Evra kutoka Senegal, Mchezaji wa klabu Manchester City, Samir Nasir kutoka Algeria na mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, pia kutoka Algeria.

Ghana ina wachezaji watatu wanaoshiriki Euro 2012.

Wachezaji ambao wangeweza kuichezea Timu ya Black Stars ni mshambuliaji Mario Ballotelli, Beki wa Ujerumani Jerome Boateng pamoja na mshambuliaji wa England, Danny Welbeck anayechezea klabu ya Manchester United.

Mzaliwa wa Tunisia akicheza kiungo Sami Khedira,anayechezea klabu ya Real Madrid ataiwakilisha Ujerumani. Luis Nani wa klabu ya Manchester United alizaliwa kwenye visiwa vya Cape Verde, ataiwakilisha Ureno.

Angelo Ogbonna ambaye wazazi wake ni kutoka Nigeria ataiwakilisha Italia.

Kwa ujumla kuna wachezaji wengi wenye asili ya Afrika kwenye mashindano ya Euro 2012 kutimiza Timu nzima ya wachezaji 11 na meza ya wachezaji wa akiba.

Hivyo, hasara ya Afrika ni ufanisi kwa Ulaya! Suali linalozuka hapa ni Je hawa wachezaji wenye asili ya Kiafrika wangeweza kufikia kiwango gani kama wangeziwailisha nchi moja ya Kiafrika kwenye mashindano haya ya Euro.