Nadal kukutana na Djokovic fainali

Nadal na Djokovic Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nadal na Djokovic

Bingwa mtetezi wa taji la Tennis ya mashindano ya kila mwaka ya Ufaransa, Rafael Nadal amefuzu kwa mara ya saba mfululizo kushiriki fainali kwa kumtwanga David Ferrer 6-2 6-2 6-1.

Mchezaji huyo ambaye ni namba mbili kwa ubora wa mchezo huo Duniani alishinda michezo mitano mfululizo kukamilisha seti ya kwanza katika dakika 39.

Nadal aliendelea kumtesa Ferrer hata wakati wa mvua iliposababisha pambano kusimamishwa.

Hali hiyo ya mateso iliendelea Nadal alipomvunja Ferrer kwa mara ya tatu kushinda seti ya tatu katika mda wa saa moja na dakika 46 na hivyo kujifungulia njia ya kupambana na hasimu wake mkuu Novak Djokovic.

Djokovic ambaye anashikilia namba ya mchezaji bora duniani alimtwanga mchezaji aliyeshikilia nambari hio kwa mda mrefu Roger Federer na kumfanya kitoweo ikiwa alimshinda hivi karibuni.

Djokovic alimshinda Federer 6-4 7-5 6-3.

Kwa ushindi huo Djokovic anakua mtu wa nne katika enzi ya Tennis ya kulipwa kushiriki fainali nne za kiwango cha grand slam.