Maria Sharapova ashinda Ufaransa

Maria Sharapova Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maria Sharapova

Maria Sharapova ameshinda mashindano ya Tennis ya Ufaransa ya mwaka huu kwa kumchapa Sara Errani wa Italia 6-3,6-2 na kujiandika katika rekodi kua mwanamke wa 10 kushinda mashindano yote ya kiwango cha grand slam.

Sharapova, mwenye umri wa miaka 25, amepata ushindi bila shida kubwa akianza kwa kushinda seti ya kwanza 6 - 3 kuongezea ngao ya Ufaransa kwenye ngao za mashindano aliyowahi kushinda ya Wimbledon, US Open na Australia.

Mrussi huyu alimzidia mpinzani wake kutoka Italia ambaye ameshiriki fainali ya grand slam kwa mara ya kwanza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Maria Sharapova

Ushindi wa Sharapova mjini Paris unamuweka kwenye kilele cha orodha ya wachezaji bora wa mchezo wa Tennis wanawake. Na kuanzia leo atachukua nafasi ya mchezaji bora duniani.

Wakati huu ambapo tennis ya wanawake ina pengo la mchezaji anayetazamwa kama nyota ya kuigwa, huenda Sharapova akawa jibu la kuziba pengo hilo.