UEFA yalaani ghasia mjini Warsaw

Mashabiki wazichapa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wazipiga

Shirikisho linalotawala soka barani Ulaya, UEFA limeshutumu ghasia zilizotokea kwenye mitaa ya mji wa Warsaw kabla ya pambano la jumanne kati ya mwenyeji mshirika wa mashindano ya Euro2012 Poland na Urussi.

Polisi imewatia mbaroni watu 184,ikiwa ni raia 156 wa Poland na Warussi 24 kufuatia mapigano makali baina ya mashabiki ambao waliwashambulia Polisi pia.

Wakuu wa nchi walikua wamejiandaa kwa uwezekano wa mtafaruku kutokea kabla ya mchuano wa jumanne ikizingatiwa kwamba uhusiano kati ya nchi hizi mbili umetiwa sumu na migogoro ya miaka mingi ikikumbukwa pia uvamizi na utekaji wa Poland kwa kipindi cha miaka 40 baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia.

Ghasia zilizuka wakati maelfu ya mashabiki wa Urussi wakisindikizwa na polisi walivuka mto Vistula wakiwa njiani kwenda uwanjani. Mapigano mengine yalizuka katikati ya mji katika eneo la mashabiki baada ya mechi iliyomalizika kwa sare ya bao moja kwa kila upande.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waliopigana wakamatwa

Waliokamatwa watahukumiwa na mamlaka inayohusika.

Mbali na matukio ya nje ya uwanja, mechi iliendelea bila tatizo ndanio ya uwanja bila kubaguana. Kinyume na ilivyo katika mechi za Ligi nyingi barani Ulaya safari hii hapakuepo wasimamizi kulinda usalama kwa kusimama katikati ya makundi ya mashabiki wanaokinzana.