Italia robo fainali

Italia na Jamhuri ya Ireland Haki miliki ya picha AFP
Image caption Italia ilicheza kwa bidii ikihofia matokeo ya mechi nyingine ya kundi C yangeliamua hatma yake

Italia ilipata ushindi dhidi ya timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa wanajitayarisha kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga magoli 2-0.

Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakin ni Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango kwanza, akitumia kichwa, kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.

Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kufunga Keith Andrews lakini kipa wa Italia Gianluigi Buffon akaweza kuokoa, ingelimaanisha Italia, katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.

Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kufunga bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.

Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.

England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.