Arsenal tayari kununua hisa zaidi

Alisher Usmanov Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Alisher Usmanov

Tajiri mmoja anayemiliki kiasi kikubwa katika hisa za klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov anasema angependa kununua hisa zaidi za klabu hio ingawa hana nia ya kupata nafasi kwenye bodi inayoongoza klabu.

Usmanov ambaye ndiye tajiri mwenye vipesa kuliko tajiri mwingine nchini jimbo la zamani la Urussi la Uzbekistan, ni mmoja wa matajiri kadhaa wanaomiliki hisa katika klabu za Uingereza kama Roman Abramovich huko Chelsea na Anton Zingarevich wa Reading.

Image caption Arsenal fc

Usmanov ameliambia shirika la habari la Reuters nje ya mji wa Petersburg kua 'daima na kwa kiwango chochote, nipo tayari kuongezea kiwango cha hisa zangu.

Usmanov, ambaye utajiri wake umetokana na biashara ya chuma na teknolojia anaweza kujijengea umaarufu na nafasi kwenye bodi kutokana na kiwango cha hisa atakazowekeza.

Chombo cha Red and White, kinachomilikiwa na Usmanov kwa ushirikiano na Farhad Moshiri,wana miliki asili mia 29.72 ya hisa katika Arsenal,kwa mujibu wa Tovuti ya klabu hio.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Stan Kroenke

Licha ya uwezo huo, Usmanov hajioni akiwa kwenye bodi ya viongozi wa Arsenal, na kwa kauli yake anasema 'singependa kuhudhuria mkutano wa bodi bila kualikwa.

Kwa mujibu wa habari za vyombo vya habari mmiliki mkubwa wa hisa za Arsenal, Kroenke anachukizwa kusikia kama Usmanov angepewa nafasi kwenye bodi ya Arsenal.