Eusebio aondoka hospitali Lisbon

Mcheza soka maarufu wa Ureno mwenye asili ya Msumbiji, aliyeichezea Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Benfica, Eusebio,ameagwa kutoka hospitali alikolazwa wakati wa kombe la Euro 2012 nchini Poland.

Image caption Kombe la Dunia 1966 England

Eusebio, mwenye umri wa miaka 70, alilazwa tena mjini Lisbon baada ya kuwaswili kutoka Poland kwa ndege ambapo hali yake haikuwaridhisha madaktari.

Mchezaji huyo mkongwe aliyepewa jina la Black Panther akiwa ni balozi wa Ureno wa soka amekuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu. Eusebio anakumbukwa mno kwa mchango wake wa mabao yaliyoiwezesha Ureno kumaliza ya tatu kwenye Kombe la Dunia la mwaka 1966 nchini England.