Machester City yaichapa Chelsea 3-2

Manchester City wameshinda kombe la Community Shield baada ya kuifunga Chelsea magoli matatu ndani ya sekunde 12 katika kipindi cha pili.

Chelsea waliongoza kwa goli moja kabla ya mapumziko wakati Fernando Torres alipochomeka goli hilo katika dakika ya 40.

Lakini Branislav Ivanovic alitolewa nje baadaye kutokana na uzembe kukabiliana na Aleksandar Kolarov.

City walichekelea baada ya Yaya Toure kuleta faraja nyumbani kwa kuchomeka goli la kwanza katika dakika ya 53 kipindi cha pili, huku Carlos Tevez akiongezea la pili sekunde sita tu baadaye katika dakika ya 59, na Samir Nasri kushindilia bao la tatu katika dakika ya 65 ikiwa ni sekunde sita tu baada ya goli la pili.

Sergio Aguero angeweza kufanya magoli 4-2 dakika moja kabla ya kuisha kwa mchezo lakini alizidiwa na mbinu.

Wakati wachezaji wengi wakijaribu kuonyesha umahiri wao kuelekea kuanza kwa msimu wa Premier League wiki hii, City ambao ni washindi wa kombe hilo msimu uliopita, walionekana kuwa mahiri zaidi kuliko wapinzani wake, ambao walishinda kombe la FA na pia la Champions League msimu uliopita.

Ushindi huu unakuwa wa kwanza kwa City toka miaka arobaini iliyopita wakiwa wameshinda kombe la FA Charity Shield mwaka 1972.