Mbio za Daimond League zachangamsha

Imebadilishwa: 26 Agosti, 2012 - Saa 17:47 GMT


Huko Birmingham mashindano ya mbio za riadha ya Diamond League yamefanyika mchana leo na bingwa wa mbio mbili wa Olympic Mo Farah ameponea chupuchupu kupitwa kabla ya kuamka na kushinda mbio za maili moja

Ummati wa watu wengi waliojitokeza kuangalia mashindano hayo walishangilia Mo Farah ambaye mke wake alijifungua mapacha wa kike siku ya Ijumaa, alishinda mbio za leo kwa kasi aliyoweka kwenye hatua ya mwisho.

Katika mbio za mita 200 mwanariadha wa Marekani Tyson Gay atafurahia matokeo baada ya kumaliza nyuma ya kijana chipukizi wa Jamaica Nickel Ashmeade aliyeshinda katika mda wa sekunde 20.12. Tyson Gay aliweka mda wa selkunde 20.21'

Carmelita Jeter alimshinda mwanamke aliyempuki kwenye Olimpiki katika mbio za mita 100 Shelly-Ann Fraser-Pryce, kwa mara ya pili katika kipindi cha siku nne akimaliza katika mda wa sekunde 10.81. Bingwa wa Olimpiki Aries Merritt hakuwa na tatizo lolote katika mbio za mita 110 kuruka viunzi aliyeondolewa kwenye mbio hizo juzi mjini Lausanne alimzidia nguvu mtani wake Jason Richardson akishinda katika mda wa sekunde 12.95.

Katika mbio nyingine kwa wanaume mbio za mita 1500: 1 Mekonnen Gebremedhin wa Ethiopia alishinda kwa mda wa dakika 3 sekunde 34 nukta 80 akifuatiwa na Nixon Kiplimo Chepseba wa Kenya na nafasi ya tatu alifuata James Kiplagat Magut, Silas Kiplagat wa (kenya akiwa wa nne na Bethwel Birgen akimaliza wa tano.

Andrew Kiptoo Rotich na Gideon Gathimba wote wa Kenya hawakumaza

Kwa upande wa wanawake Mariya Savinova wa Urusi alishinda mbio za mita 800 akifuatiwa na Pamela Jelimo wa Kenya na Marilyn Okoro wa Uingereza akiwa wa tatu na Winny Chebet akamaliza wa sita.

Kwa upande wa wanawake Mariya Savinova wa Urusi alishinda mbio za mita 800 akifuatiwa na Pamela Jelimo wa Kenya na Marilyn Okoro wa Uingereza akiwa wa tatu na Winny Chebet akamaliza wa sita.

Katika mbio za mita elfu tatu kwa kina dada Mk wakenya walichukua nafasi za kwanza tano. Mercy Cherono aliiubuka mshindi kwa kutumia mmuda wa dakika nane sekunde 41 nukta 21 akifuatwa na mshindi wa medali ya shaba katika mechezo ya olimpiki Vivian Cheruiyot na Sally Kipyego.

Viola Jelagat naye alimaliza katika nafasi na nne huku veronica Nyarwai naye akimaliza katika nafasi ya tano.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.