Kocha wa Kuwait apigwa risasi

Imebadilishwa: 26 Agosti, 2012 - Saa 18:57 GMT

Goran Tufegdzic

Polisi ya Serbia inasema kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Kuwait Goran Tufegdzic ameuawa kwa kupigwa risasi nchini mwao Serbia na hali yake imesemekana ni mbaya.

Polisi katika mji wa Pozarevac ulio katikati mwa nchi wamesema kuwa Bw.Tufegdzic alipigwa risasi ya kifua siku ya ijumaa baada ya ugomvi na jirani juu ya kipande cha ardhi. Baada ya hapo alimpiga risasi na kukimbizwa hadi hospitali ya mjini Belgrade.

Tufegdzic, ambaye amefanya kazi huko Mashariki ya kati kwa takriban miaka kumi aliteuliwa kama kocha wa Kuwait mwaka 2009. Aliiwezesha timu hio kufuzu kushiriki kombe la mataifa ya bara Asia la mwaka 2010 na kuisaidia kushinda kombe la mataifa ya Ghuba la mwaka 2010.

Mwenyekiti wa chama cha mpira cha Kuwait Sheik Talal Al-Sabah anasema kuwa amezungumza na mke wa kocha huyo na ana matumaini atapata nafuu na kwamba familia yake itaweza kupitia kipindi hiki kigumu''

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.