Rudisha harudi nyumbani hadi msimu uishe

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 18:33 GMT

David Rudisha

Mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake anatumaini la kutenda maajabu atakaposhiriki mbio za Diamond League mjini Zurich siku ya Alhamisi.

Alipokimbia mjini Lausane wiki iliyopita katika mbio za mita 100 aliweka mda mzuri ila tu Bolt ndiye ana mda bora kuliko.

Blake, aliyeshinda medali za fedha katika mbio za mita 100 na 200 wakati wa Olimpiki ataongoza orodha ya washindi wa medali za dhahabu 15 mjini London 2012.

Hata hivyo bingwa huyu wa Dunia hatoshindana na Bolt baada ya kukubaliana kuwa hawatoshindana baina yao kwa kipindi cha msimu kilichosalia. Bolt ana mipango ya kukimbia mita 200 kwenye uwanja wa mjini Zurich wa Letzigrund.

Blake, aliyeingia msimu huu akiwa na mda wa 9.82 kutoka mashindano ya Zurich ya mwaka jana aliweka mda mzuri msimu huu wa 9.75 kabla ya kunyoa sekunde nyingine huko Lausanne na kuweka sekunde 9.69 mjini Lausanne, hapo kesho atashindana na Tyson Gay pamoja na Ryan Bailey wote wa Marekani.

Mshindi wa medali sita za Olimpiki Usain Bolt, aliyeweka mda wa sekunde 19.58 mjini Lausanne atapambana na mwananchi mwenzake Warren Weir, aliyeshinda medali ya shaba kwenye Olimpiki za London na vilevile Jason Young.

Kwingine David Rudisha, aliyevunja rekodi ya mbio za mita 800 duniani kabla ya kushinda medali ya dhahabu mjini London atashiriki mashindano pekee kufuatia mashindano ya Olimpiki mjini London.

Rudisha ambaye tangu wakati huo hajarudi nyumbani ana imani ya kuweka mda mzuri.

Alielezea sababu yake ya kutorudi nyumbani kama kutaka kujiweka katika hali ya ushindani bila kupoteza mazowezi, Lau kama ningekwenda nyumbani ningewekwa katikati ya vivutio ya sherehe na nisahau kua kuna mazowezi." Rudisha aliiambia BBC. "kwa hiyo ilibidi nikae Ulaya kuhitimisha msimu kisha nitarudi nyumbani nisherehekee.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.