Theo Walcott haondoki Arsenal

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 17:42 GMT

Theo Walcott

Habari mpya zilizochomoza punde zasema Theo Walcott yumkini haondoki Arsenal majira haya baada ya mazngumzo ya faragha na meneja wa Arsenal Arsene Wenger mapema leo jumatano.

Inafahamika kuwa kijana huyo ametoa ahadi kwa kauli ingawa hajatia saini mkataba mpya wa kudumu na atatakiwa kufanya hivyo.

Arsenal iliamua kumpa nyongeza kwa kukubali kitita cha pauni za Uingereza cha pauni 75,000 kwa kila wiki kwa kipindi cha miaka mitano ya mkataba lakini akakataa na baada ya hapo imedhihirika kuwa mchezaji huyo pamoja na kuomba mshahara mkubwa anataka abaki kuichezea Arsenal.

Mabadiliko haya yamekuja baada ya kijana Walcott kuzungumza na Meneja wake wakati wa mazowezi kwenye uwanja wa Colney, ambapo Wenger aliridhika na moyo wa kijana kutaka kuendelea kuchezea klabu.

Awali Arsenal ilikuwa tayari kumuuza mchezaji huyo asipokubalia kutia saini mkataba mpya kabla ya siku ya Ijumaa.

Mchezaji huyo mwenye sifa ya kasi kwenye upande wa kulia wa uwanja ana mda wa mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Arsenal.

Tangu aondoke aliyekuwa nahodha msimu uliopita, Robbin Van Persie, Walcot aliyesajiliwa kutoka klabu ya Southampton kwa kitita cha pauni milioni 9.1anaonekana kuwa aliyetetereshwa na kuondoka kwa nahodha huyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.