Jenson Button ashinda mbio za Ubelgiji

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 15:56 GMT

Jenson Button akisherehekea ushindi

Dereva muingereza Jenson Button amejiweka katika nafasi nzuri ya kushinda ubingwa wa Dunia wa mashindano ya magari Formula One baada ya kushinda mbio za Grand Prix za Ubelgiji.

Hii ni baada ya Button kuepuka mkosi uliowakumba madereva wenzake wanne katika kona ya kwanza.

Katika mashinano hayo Bingwa Fernando Alonso ndie aliyepata hasara kubwa zaidi baada ya gari lake kupindukia katika hatua za kwanza . Ajali hiyo imemzima Alonzo kuwa kiongozi wa mashindano hayo ya langalanga kwa mashinano 23 mfululizo. Mkosi huo pia ulimkumba Dereva wa kampuni ya magari ya McLaren, Lewis Hamilton.

Ajali hiyo ilisababishwa na dereza wa magari ya Lotus , Romain Grosjean. Na hii sio mara ya kwanza kwa gereva huyo kusababisha ajali katika mashindano hayo. Naye dereva Sergio Perez alilazimika kujiondoa kwenye mbio hizo

Ushindi huu wa leo wa Button ni wa 14 kwa dereva huyo hivyo kumfanya awe mbele ya dereva Alonzo kwa pointi 63 hii sasa inampea Button kuwa na tamaa ya kusinda ubingwa ya mbio hizo za magari mwaka huu.

Bingwa mteteza Sebastian Vettel, ambaye alianza akiwa katika nafasi ya 10 ambaye amekuwa hafanyi vizuri , hii leo ameibuka wapili. Hii sasa inamaanisha Vettel yuko nyuma ya laonzo kwa pointi 24 pekee.

Dereva mwengine Kimi Raikkonen wa magari ya Lotus ni wanne , pointi mmoja nyuma ya Mark Webber ambaye anashikilia nafasi ya tano.

Fernando Alonso

Dereva wa timu ya magari ya Ferrari Fernando Alonso pamoja na wa timu ya McLaren,
Lewis Hamilton wameondoka kwenye mashindano ya mbio za magari ya Ubelgiji mapema leo.

Gari la tahadhari lililetwa haraka kabisa baada ya ajali kwenye kona ya kwanza iliyosababisha kustaafu mapema kwa dereva wa timu ya magari ya Sauber, Sergio Perez kutoka Mexico na Mfaransa Romain Grosjean.

Picha za runinga zilionyesha kuwa gari la Grosjean, lilipaa angani na kuangukia pua ya gari la timu ya Ferrari nalo likainuka na kuelekea gari la Muingereza Hamilton ambaye alishindwa kuendelea.

Mabaki ya magari hayo yalitapakaa kwenye barabara.

Alonso alitazamia kufikia rekodi ya mashindano haya inayoshikiliwa na Michael Schumacher ya kuzoa pointi 24 mfululizo kwa kumaliza kila mbio anazoshiriki na kwa sasa anaongoza kwa pointi 40 mbele ya mtani wake wa magari ya Red Bull Mark Webber kukiwa na mbio 8 zilizosalia.

Alonzo ambaye ni lazima amshukuru Mngu kwa kuyanusuru maisha yake bila gari lile kumgonga kichwa alikaa ndani ya gari lake kwa mda bila kutoka ingawa hali yake ni nzurio wala hana jeraha.

Kamui Kobayashi wa Japan aliyefanya mabadiliko ya tairi na mafuta punde baada ya ajali hio alirejea na kuanza mwisho wa magari yote huku Jenson Button wa magari ya McLaren akiongoza mbio hizi.

Uchunguzi unaendelea kuhusu ajali hio.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.