Denmark sare na Czech

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 20:58 GMT

Denmark na Czech zatoka sare

Timu ya Denmark ilitoka sare bila ya kufungana bao lolote na wageni wao Jamhuri ya Czech katika mechi iliyochezwa siku ya jumamosi.

Hii ilikuwa ni kutafuta nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la dunia , nchini Brazil mwaka 2014.

Katika kipindi cha kwanza Denmark ilifanya mashambulizi makala katika lango la Czech lakini bila mafanikio.

Na kipindi cha pili ikawa zamu ya Czech kufanya mashambulizi ambayo pia hayakuzaa matunda.

Japo katika dakika za mwisho wa mechzo huo Denmark ilipiga kambi katika lango la Czech lakini kipa Petr Cech alihakikisha mpira umemalizika kwa 0-0.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.