England yaifunza Moldova mpira

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 21:17 GMT

Mwamba Frank Lampard akifumua shuti kali

England iliipa Moldova kichapo cha mabao 5-0 siku ya Ijumaa katika uwanja wa Chisinau, Moldova.

Timu hiyo ya Moldova,ambayo haina historia ya kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa ilihangaishwa kuanzia dakika ya mwisho na England.

Kabla ya kwenda mapumzikoni vijana wa Meneja Roy Hodgson walikuwa kifua mbele kwa magoli 3-0.

Goli la kwanza lilifungwa na Frank Lampard kwa njia ya penalti katika dakika za kwanza kwanza kabla wa mwamba huyo wa Chalsea kufanya mambo kuwa 2-0 alipofunga kwa kichwa .

Baadae mshambulizi Jermain Defoe aliipatia Englanda bao la tatu.

Ilimlazimu James Milner wa Man City kusubiri hadi dakika ya 16 kabla ya kuipatia Englanda la nne kabla ya Leighton Baines kufunga ukurasa wa magoli.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.