Chipolopolo yailipua Cranes

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 19:17 GMT

Nahodha Christopher Katongo asherehekea goli

Mabingwa wa Afrika Zambia wamewafunga Uganda bao 1-0 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Levy Mwanawasa , mjini Ndola ,zambia, Jumamosi.

Hii ilikuwa mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la Afrika za mwaka 2013, Afrika kusini.

Nahodha wa Chipolopolo Christopher Katongo alifunga goli kutokea katikati ya uwanja kipindi cha kwanza cha mchezo.

Mchezaji huyo anayesakata soka ya kulipwa nchini China alitumia mwanya wa kuzubaa kwa mabeki wa The Cranes kunasa mpira wa kurusha wa Davies Nkausu na kufurahisha mashabiki wapatao 40,000 waliohudhuria mechi hiyo.

Uganda, inasaka nafasi kwa mara ya kwanza kucheza fainali za kombe la Afrika (AFCON) tangu mwaka 1978 ilipomaliza mshindi wa pili nyuma ya wenyeji Ghana.

Timu hizo mbili zitarudiana nchini Uganda katikati ya mwezi Oktoba, mwaka huu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.