Lewis Hamilton ashinda Italia

Imebadilishwa: 9 Septemba, 2012 - Saa 14:34 GMT

Lewis Hamilton wa McLaren

Katika mashindano ya mbio za magari ya Langalanga ya huko Italia mapema leo ambako Muingereza Lewis Hamilton wa Timu ya magari ya McLaren ameshinda mbio hizo kwa mara ya kwanza tangu aanze kushiriki mashindano haya na kuandika ushindi wake wa pili katika mbio tatu za mwisho.

Bila shaka Lewis Hamilton alitazamiwa na wafuatiliaji wengi wa mbio za magari ya Langalanga baada ya wiki iliyopita kujikuta katika ajali kwenye kona ya kwanza na baada ya kujishindia nafasi ya kuanza mashindano haya mbele ya Madereva wenzake, ilibidi afuate mfano wa mshindi wa mbio zilizopita za Ubelgiji Jenson Button.

Na hivyo ndivyo alivyofanya kumaliza kama alivyoanza, mbele ya Madereva wenzake na kuepuka purukushani ya aina yoyote wala mkwaruzano na madereva wengine.

Nyuma yake kilikuepo kivumbi, ambako Dereva wa timu ya magari ya Sauber, Sergio Perez kutoka Mexico aliyeanza katika nafasi ya 12 alipoendesha gari kama aliyekumbwa, na hadi mzunguko wa mwisho alikua ameisha punguza kiasi cha sekunde nyingi kufikia sekunde 11 nyuma ya mshindi Hamilton.

Sergio Perez wa Sauber

Dereva anayeongoza kwa wingi wa pointi Fernando Alonzo wa magfari ya Ferrari alimaliza wa tatu na hivyo kuongezea pointi zake na kuzidisha pengo kati yake na Hamilton....ya 37 zikisalia mbio saba kuhitimisha msimu.

Bingwa mtetezi wa mashindano haya Sebastien Vettel wa magari ya Red Bull ambaye alikua mpinzani wa karibu wa Alonzo kuwania ubingwa, alishindwa kumaliza zikisalia raundi ya sita kabla ya mwisho wa mbio.

Mshindi wa mbio za Ubelgiji, wiki iliyopita, Jenson Buttyon wa magari ya McLaren pia hakumaliza mbio za leo.

Hivyo Lewis Hamilton bakamaliza wa kwanza kwenye mashindano ya mbio za leo na kukusanya jumla ya pointi 142 akiwa nyuma ya Fernando Alonzo mwenye pointi 179 , Kimmi Raikonen ni wa tatu akiwa na jumla ya pointi 141.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.