Murray bingwa US Open

Imebadilishwa: 11 Septemba, 2012 - Saa 08:22 GMT
Andy Murray

Huu ni ushindi wa kwanza wa Uingereza wa mashindano makubwa ya Grand Slam baada ya miaka 76

Andy Murray hatimaye aliiwezesha Uingereza kupata ushindi katika mashindano makubwa ya tennis ya Grand Slam, baada ya kusubiri miaka 76, baada ya kumshinda Novak Djokovic katika mashindano ya US Open.

Murray, mwenye umri wa miaka 25, aliiga yale aliyoyafanya Fred Perry, mwaka 1936, aliposhinda 7-6 (12-10) 7-5 2-6 3-6 6-2 katika muda wa saa nne, dakika 54 katika uwanja wa Arthur Ashe.

Murray pia alifanikiwa kuingia fainali ya Wimbledon, na baada ya kutokwa machozi kufuatia kushindwa, alijitahidi katika fainali ya Olimpiki, na akapata medali ya dhahabu.

"Nilipotambua nimeibuka mshindi, nilikuwa kidogo nimeshituka. Nilijihisi angalau nikipumua, na hisia nyingi zilinijia,” alieleza Murray.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.