Bondia Hatton kurudi ulingoni

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 15:37 GMT
Ricky Hatton

Hatton alipokonywa leseni kutokana na madai ya kutumia dawa ya kulevya

Ricky Hatton, bondia wa Uingereza ambaye zamani alikuwa ni bingwa wa dunia katika viwango viwili vya uzani tofauti, inaelekea huenda leseni yake ya kurudi katika ngumi ikaidhinishwa hivi karibuni.

Hatton, mwenye umri wa miaka 33, alihudhuria kikao cha bodi ya ngumi, British Boxing Board of Control (BBBoC), mjini Cardiff, siku ya Jumatano, na anatazamiwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari Ijumaa.

Katibu mkuu wa bodi, Robert Smith, aliielezea BBC kwamba: "Leseni yake atarudishiwa, mara tu baada ya kukaguliwa hali yake ya afya.

"Alizungumza vyema, anaonekana kuwa mwenye afya nzuri, na angelipenda kwa mara nyingine kushangiliwa."

Hatton, ambaye alibandikwa jina la utani 'The Hitman', yaani 'mgongaji', hajawahi kupigana tena tangu aliposhindwa kwa KO katika raundi ya pili, alipotandikana na Manny Pacquiao mwezi Mei, mwaka 2009.

Mwaka 2010, bodi hiyo ya ngumi ilimpokonya Hatton leseni, kufuatia madai ya kutumia dawa ya kulevya ya cocaine.

"Anaonekana yuko katika hali nzuri kabisa, hana shida yoyote, na inaelekea hana matatizo yoyote," alielezea Smith.

"Kutokana na matamshi yake, inaelekea ametulia vyema na familia yake. Tayari ameshapitia ukaguzi fulani wa kimatibabu, na tumo katika kuhakikisha anakamilisha utaratibu mzima."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.