Chama hakijiwezi Sierra Leone

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 17:30 GMT
Paul Kamara

Waziri wa michezo Kamara amevunjilia mbali bodi ya shirikisho la soka nchini Sierra Leone

Mzozo katika chama ulizidi wiki iliyopita, wakati waziri wa michezo, Paul Kamara, aliilaumu bodi ya SLFA kwa uzembe, na akaivunjilia mbali.

Lakini ilipofahamika kwamba shirikisho la FIFA lilikuwa likiangalia hali iko vipi, na kulikuwa na uwezo wa kuipiga timu ya Sierra Leone marufuku isicheze katika mechi za kimataifa, rais Ernest Bai Koroma aliamuru bodi ya SLFA irudishwe kazini.

Kufuatia hayo, FIFA ilisitisha uchaguzi uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki, na ikamtuma Corvaro katika taifa hilo la Afrika Magharibi, kuzungumza na wahusika wote.

Kulingana na Corvaro, kuna "hali ya watu waliopo katika Kamati ya Rufaa ambao hawana uhalali wowote katika kuwa hapo, maanake hawakuidhinishwa vyema, na tayari wameamua kauli fulani kuhusiana na utaratibu wa uchaguzi."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.