Ian Poulter atazamia ushindi golf

Imebadilishwa: 26 Septemba, 2012 - Saa 15:50 GMT
Ian Poulter

Poulter anasema mashindano ya Kombe la Ryder ni ya kusisimua sana

Akizungumza kutoka Medinah, jimbo la Ilinois, Marekani, mchezaji kutoka Uingereza, Ian Poulter, ameelezea kwamba yeye hupata msisimko zaidi katika mashindano ya Kombe la Ryder, akiyalinganisha na mashindano mengine kote duniani.

Siku ya Jumatano pia ameelezea shauku ya kulitaka kombe hilo mno.

"Sote ni marafiki wazuri, upande huu na ule mwingine wa kisima", alielezea Poulter.

"Lakini kuna jambo fulani katika mashindano ya Kombe la Ryder ambalo hunisisimua, jinsi mnavyoweza kuwa marafiki wakubwa, lakini katika mashindano ya Kombe la Ryder, ukataka kuwaua. Ni mashindano ya kusisimua sana, na hisia ambazo huzijui hujitokeza."

Hii itakuwa ni mara yake ya nne kushiriki katika mashindano hayo.

Kati ya mara tatu aliposhindwa, alibwagwa na Tiger Woods.

Poulter amepuuza wazo kwamba Rory Mcllroy ni mtu ambaye ataandamwa sana Medinah kwa kuwa ndiye nambari moja duniani, na bingwa mara mbili katika mashindano mawili makubwa.

Poulter anaamini kwamba wachezaji wote 12 katika timu ya Ulaya ni mahiri, na yeyote anaweza kuibuka mshindi.

Nahodha wa timu ya Ulaya ni raia wa Uhispania, Jose Maria Olazabal, na atakiongoza kikosi cha Ulaya katika mashindano hayo ambayo yanaanza Ijumaa, tarehe 28 Septemba.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.