Chelsea yaichapa Arsenal kwao

Imebadilishwa: 29 Septemba, 2012 - Saa 14:28 GMT

Kiper wa Arsenal Vito Mannone afungwa

Chelsea imekuwa timu ya kwanza kuichapa Arsenal katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa 1-2 katika uwanja wao wa nyumbani,Emirates siku ya Jumamosi.

Vijana wa Roberto Di Matteo ndio walikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi Fernando Torres baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.

Lakini katika dakika ya 42 mshambulizi Gervinho alifunga bao safi hivyo kuzifanya timu hizo mbili ziende mapumzikoni zikiwa sare ya 1-1.

Na katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili, Mata alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo ulimshinda mlinzi Laurent Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia ndani huku ikimuacha Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi.

Wenger amekua akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya adhabu.

Licha ya kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya mbele ya vijana hao wa Arsene Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na kukosa umakini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.