Chelsea yailima Arsenal 2-1

Imebadilishwa: 29 Septemba, 2012 - Saa 14:55 GMT
Chelsea

Chelsea bado imo kileleni katika ligi kuu ya Premier

Chelsea inaendelea kuongoza katika ligi kuu ya Premier, baada ya siku ya Jumamosi kuishinda Arsenal, ambayo ilikuwa ikichezea uwanja wa nyumbani wa Imarati, magoli 2-1.

Hii ni mara ya kwanza msimu huu kwa Arsenal kushindwa ikichezea uwanja wa nyumbani.

Nahodha wa Chelsea, John Terry, aliweza kucheza katika mechi hiyo, huku akiwa bado anawaza kama atakata rufaa au la, baada ya chama cha soka cha England cha FA, kumpiga marufuku ya mechi 4, na kumtoza faini ya pauni 220,000, kwa kumpata na hatia ya kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand.

Ushindi wa Chelsea ulipatikana kupitia bado la mapema la Fernando Torres, ambaye aliweza kunyemelea nyuma ya Laurent Koscielny, na kuusindikiza mkwaju wa free-kick kutoka kwa Juan Mata.

Gervinho aliweza kuisawazishia Arsenal kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, lakini vijana wa Roberto Di Matteo walitwaa pointi zao tatu katika kipindi cha pili, wakati mpira wa free-kick kutoka kwa Mata uliweza kumgusa kidogo tu Koscielny na kukifanya kibarua cha kipa wa Arsenal, Vito Mannone, kutoweza kuufikia mpira huo.

Mechi hii ni kipimo kizuri kwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, kuipima timu yake, na kudadisi ikiwa ina uwezo wa kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Premier msimu huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.