Olazabal amkumbuka Seve Ballesteros

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 13:13 GMT
Jose Maria Olazabal

Olazabal alimkumbuka marehemu Seve Ballesteros timu ya Ulaya ilipopata ushindi wa Kombe la Ryder

Nahodha wa timu ya golf ya Ulaya, Jose Maria Olazabal, alimkumbuka marehemu Seve Ballesteros, mchezaji maarufu wa golf wa Uhispania, wakati timu yake ilipopata ushindi wa pointi 14½ dhidi ya 13½, ilizopata timu ya Marekani, katika ushindi wa Kombe la Ryder katika uwanja wa Medinah, nchini Marekani.


Olazabal, akishirikiana na Mhispania mwenzake Ballesteros, walikuwa ni wachezaji walioweza kuimarisha timu ya Ulaya mno, wakati siku hizo Ballesteros akiwa mchezaji mahiri.

Ballesteros aliaga dunia mwezi Mei, mwaka 2011.

"Timu yetu ilicheza kikamilifu kutokana na kumbukumbu za Seve, na pasipo kukata tamaa," alieleza Olazabal.

"Mliamini yatawezekana, na nashukuru mlifanikiwa, na ni fahari yangu kwamba mikono yenu imeiwezesha Ulaya kuendelea kulishikilia Kombe la Ryder."

Olazabal na Ballesteros, wakishirikiana kwa pamoja kama wachezaji wawili mahiri, siku zao waliweza kupata pointi 12, katika mechi 15.

"Seve siku zote atakuwa pamoja na timu hii, na alikuwa na mchango muhimu katika shindano hili.

"Vijana walielewa kujiamini ni jambo muhimu sana, na hivyo ndivyo walivyofanya. Kwa watu 12 wa bara Ulaya, mlichofanya uwanjani ni jambo la ajabu," alieleza Olazabal.

Ballesteros aliweza kushiriki mara 8 katika mashindano hayo ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili, na aliweza kuiongoza timu kama nahodha wakati ilipoibuka bingwa katika uwanja wa nyumbani Uhispania, mwaka 1997.


BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.