CAF yatangaza majina 34

Imebadilishwa: 5 Oktoba, 2012 - Saa 12:30 GMT

Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, limetoa orodha ya wachezaji 34 ambao watawania tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka katika bara hilo mwaka 2012.

Timu ya Zambia

Wachezaji wawili kutoka timu ya taifa ya Zambia ni kati ya wale watakaowania tuzo

Kati ya wachezaji hao, ni mchezaji Yaya Toure, kutoka Ivory Coast, na ambaye huichezea klabu ya Uingereza ya Manchester City.

Toure alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka uliopita.

Katika orodha hiyo, wamo wachezaji watatu ambao huvichezea vilabu vya Afrika.

Wachezaji wawili wa Zambia, Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu, wote ni wachezaji wa klabu ya TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na Youssef Msakni kutoka Tunisia ni mchezaji wa Esperance.

Msakni hata hivyo anatazamiwa kuihama Esperance, na kuelekea Qatar mwezi Januari mwaka ujao, kujiunga na klabu ya Lekhwiya.

Kalaba na Sunzu tayari wana sifa za kutosha, baada ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Zambia kuibuka mabingwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Gabon.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.