Cole ashtakiwa na FA

Imebadilishwa: 8 Oktoba, 2012 - Saa 13:08 GMT
John Terry na Ashley Cole

Cole anaadhibiwa kwa kuandika maneno yasiyofaa dhidi ya chama cha soka cha FA

Ashley Cole ameshtakiwa na chama cha kandanda cha England cha FA, kutokana na ukosefu wa nidhamu, kufuatia na maneno aliyoyaandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter, kuhusiana na usimamizi wa chama hicho.

Akiandika baada ya uamuzi wa chama hicho cha soka kumuadhibu John Terry katika kesi juu yake ya ubaguzi wa rangi, Ijumaa iliyopita aliandika: "Hahahahaa, vyema kabisa...FA, nilidanganya?...kundi la ....***".

Mchezaji huyo, ambaye ni mlinzi wa klabu ya Chelsea, na mwenye umri wa miaka, 31 alikuwa Jumatatu ajiunge na timu ya taifa ya England.

Cole ana nafasi ya kujitetea juu ya kosa hilo la kukosa nidhamu, kabla ya saa kumi, Alhamisi, tarehe 11 Oktoba.

Cole aliandika maneno hayo kufuatia uamuzi wa tume huru ya FA, ambayo ilimpata John Terry na hatia ya kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR msimu uliopita.

Baadaye Cole alikiomba radhi chama cha FA.

Mbali na kufuta maneno aliyoyaandika, aliandika taarifa ikielezea: "Nilikuwa nimemaliza mazoezi tu nilipoyaona yale yaliyotangazwa katika televisheni kuhusiana na niliyoyasema juu ya chama cha FA.

"Yalinisikitisha mno, kwani nilikuwa nimeandika hisia zangu kwa haraka katika joto la matukio hayo. Ninakiomba radhi mno chama cha FA kwa maneno yangu."

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England, Alan Shearer, mwishoni mwa wiki alisema inafaa Cole apigwe marufuku asicheze mechi ya Ijumaa ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, dhidi ya San Marino.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.