Papa Diop aingia Birmingham City

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 18:27 GMT

mchezaji Papa Bouba Diop

Birmingham City imesaini mkataba wa muda mfupi na mchezaji Papa Bouba Diop.

Baada ya kufanya mazoezi na timu ya Chelsea kwa wiki kadhaa zilizopita, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 34 amefaulu katika vipimo vya afya na atatia saini mkataba wa mwezi mmoja, wakati maombi ya visa yake yakisubiriwa.

Diop alijenga jina lake katika soka la England baada ya kujiunga na Fulham akitokea timu ya Lens ya Ufaransa mwaka 2004.

Aliichezea timu hiyo kwa misimu mitatu akiwa na Fulham, ambako alicheza pamoja na boss wa Chelsea, Lee Clark.

Baada ya hapo alihamia timu ya Portsmouth mwaka 2008, ambako alishinda kombe la FA katika msimu wake wa kwanza katika timu hiyo.

Akiwa amenyakua kombe la Ugiriki mwaka 2011 akiichezea timu ya AEK Athens, alirejea England msimu uliopita akijiunga na West Ham.

Aliichezea timu hiyo mara 16 lakini baada ya Desemba hakupatiwa nafasi kubwa ya kuichezea timu hiyo na kuachwa msimu huu wa majira ya joto.

Diop aliiwakilisha Senegal mara nne katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo iliyofikia hatua ya robo fainali katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002, zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Japan na Korea Kusini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.