Andy Murray amshinda Radek Stepanek

Imebadilishwa: 13 Oktoba, 2012 - Saa 16:26 GMT
Andy Murray

Murray amefuzu kuingia fainali ya Shanghai Masters

Andy Murray baada ya kulemewa kwa seti moja, hatimaye alifanikiwa kujitahidi na kumshinda mchezaji wa Jamhuri ya Czech, Radek Stepanek, 4-6 6-2 6-3 katika robo fainali ya mashindano ya Shanghai Masters.

Murray, mwenye umri wa miaka 25, na kutoka Uskochi, amejiweka katika nafasi nzuri ya kupata ushindi mkubwa mara tatu mfululizo.

Murray, bingwa wa tennis katika mashindano ya Olimpiki na yale ya Marekani ya US Open, alionyesha kuchukizwa na kuitupa raketi chini kwa hasira.

Lakini aliweza kujikakamua na kufanya vyema baadaye.

Murray alisema: "Niliweza kuinua kiwango changu cha mchezo. Yeyote angeliweza kuibuka mshindi."

Katika kipindi cha miaka mitatu, Murray amewahi kushinda katika mapambano 11 ya Shanghai, mawili akavukuka kwa wapinzani kutocheza, na kushindwa katika mawili.

Stepanek ameshawahi kumshinda Murray mara moja tu, licha ya kukutana katika mapambano matano.


BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.