'Messi' wa Liverpool ni Luis Suarez

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 14:14 GMT
Luis Suarez

Brendan Rodgers amemfananisha na Lionel Messi wa timu ya Barcelona

Meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers, amesema mshambulizi wa timu yake Luis Suarez anaweza kufananishwa na Luis Suarez, kufuatia bao zuri la kupendeza mno, na la kusawazisha, walipoikaribisha Newcastle siku ya Jumapili.

Suarez alifunga bao hilo la kusisimua mno katika uwanja wa Anfield.

"Anacheza kama mchezaji nambari tisa asiyefahamika vyema yuko wapi, kama anavyofanya Messi katika klabu ya Barcelona, na anapocheza huru na wachezaji wa upinzani inabidi kumfuata nyuma kwa kasi anapojipenyeza kati yao," Rodgers aliielezea kampuni ya matangazo ya televisheni ya Sky.

Suarez hasa ndio aliisababishia timu ya upinzani matatizo makubwa, mara kwa mara akiishambulia Newcastle, na wakati mwingi akicheza katikati ya uwanja, na hata pia katika eneo la ulinzi.

Liverpool tayari walikuwa wamelemewa wakati Yohan Cabaye alipotangulia kufunga, kabla ya Suarez hatimaye kusawazisha katika kipindi cha pili.

"Tulivunjika moyo tuliposhindwa kupata ushindi," aliongeza Rodgers.

"Tulipata nafasi za kutosha kupata ushindi, lakini sina malalamiko kuhusiana na hayo.

"Mara tu tutakapoweza kupata wachezaji wa kiwango hicho na wanaoweza kufikia hadi ya mchezo wetu, basi tutakapoweza kuwika katika mechi kama hiyo tutakuwa na nafasi bora zaidi."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.