Manchester United yapunguza deni

Imebadilishwa: 14 Novemba, 2012 - Saa 15:02 GMT
Manchester United

Inaendelea kupunguza deni

Klabu ya soka ya Manchester United imepunguza deni lake katika robo ya kwanza ya mwaka huu, baada ya familia ya Glazer inayomiliki timu hiyo, kulipa milioni 62.6.

Kwa jumla, deni lilipungua na kusalia pauni milioni 359.7, katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe 30 mwezi Septemba, mwaka 2012.

Deni hilo limepungua kwa asilimia 17, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.

Mapata ya Manchester United yalipanda kwa asilimia 3.4, na kufikia faida ya pauni milioni 76.3, klabu hiyo ya Old Trafford imeelezea.

Lakini faida kutokana na utangazaji wa mechi zake ilipungua kwa asilimia 37.4, na kufikia pauni milioni 13.7, hasa kutokana na kubadilishwa kwa ratiba za mechi.

Klabu kilicheza mechi moja ya klabu bingwa, ilhali msimu uliopita ilicheza mechi mbili, na vile vile ilipungukiwa kwa mechi mbili zilizotangazwa moja kwa moja, ikilinganishwa na msimu wa awali.

Tofauti hizo zilisababisha hasara ya pauni milioni 5.6, ilhali klabu kina matumaini kitakuwa katika hali bora zaidi kwa kucheza mechi zaidi za klabu bingwa.

Manchester United ilipungukiwa kwa milioni 2.6, kwa kucheza mechi chache za klabu bingwa, hasa kwa kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Premier, msimu 2011-12, ilikilinganishwa na msimu 2010-11.

Klabu, kwa sasa kinaongoza katika ligi kuu ya Premier.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.